Mafuriko yauwa watu wasiopungua 33 Kinshasa
7 Aprili 2025Takriban watu 33 wamekufa baada ya mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kinshasa kukumbwa na mafuriko.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo mapema leo Jumatatu iliandika ujumbe kwenye ukurasa wa X ikisema wahanga hao, walifariki kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoleta uharibifu mkubwa na kusomba majumba na kuwaacha wakaazi wengine wakifunikwa na maji.
Mvua yasababisha vifo na maafa KongoTaarifa zinasema mto Ndijili ambao unapitia mjini Kinshasa nao pia ulifurika na kupasua kingo zake siku ya Jumamosi usiku. Takriban watu 50 wako hospitali na inaelezwa kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka , huku maafisa wa uokoaji wakijaribu kuyafikia maeneo yasiyo na mawasiliano kutokana na mafuriko.
Watu walioachwa bila makaazi wanaendelea kujihifadhi kwenye uwanja wa michezo kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani huku mitaa mingi ya Kinshasa bado ikiwa imefurika maji.