MigogoroMashariki ya Kati
Watu 20 wamekufa Gaza baada ya lori la misaada kupinduka
6 Agosti 2025Matangazo
Bado haijafahamika wazi ikiwa tukio hilo lilikuwa ajali au ikiwa watu waliokuwa wakitafuta msaada ndio walisababisha lori hilo kupinduka.
Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya raia wanaokabiliwa na njaa walikuwa wamekusanyika ili kupokea msaada wa kibinadamu, na ndipo jeshi la Israelliliamuru lori hilo kupita njia isiyo salama.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Palestina WAFA, watu 1,568 ndio wamepoteza maisha wakati wakisubiri msaada huku wengine zaidi ya 10,000 wakijeruhiwa.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, malori mengi ya misaada huporwa na raia wenye njaa pamoja na makundi yenye silaha mara tu yanapoingia Gaza na hata kabla ya kufika eneo husika, jambo ambalo mara nyingi husababisha machafuko na matukio ya hatari.