Takriban watu 10 wauawa katika shambulizi nchini Nigeria
21 Juni 2025Msemaji wa polisi Nahum Daso, ameliambia shirika la habari la AP kwamba, mripuko huo ulitokea katika eneo la Konduga linalopatikana takriban kilomita 30 kutoka Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno.
Mkazi mmoja wa Konduga Ismail Ahmed, amesema mshambuliaji huyo alifanikiwa kupenya bila kutambuliwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Amnesty yazikosoa serikali kushindwa kuwalinda raia duniani
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa mshambuliaji alikuwa mwanamke na kwamba waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali iliyo karibu ili kupatiwa matibabu.
Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limekumbwa na mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa makundi ya itikadi kali ya Boko Haram na lile linalojiita dola la kiislamu, IS.