Mashambulizi ya Israel yawaua watu 10 Ukanda wa Gaza
11 Mei 2025Kwa mujibu wa Hospitali ya Nasser iliyopokea miili ya waliouwawa kwenye mashambulizi hayo mjini Khan Younis, mashambulizi mawili yaliyalenga mahema na kila shambulio liliwauwa watoto wawili na wazazi wao.
Soma zaidi: Israel yaidhinisha operesheni mpya ya kijeshi kuitwaa Gaza
Shambulio jingine limemuuwa mtoto mmoja na mengine yameripotiwa kuwauwa mtoto na mwanamume aliyekuwa akiendesha baiskeli.
Kuhusu mashambulizi hayo, jeshi la Israel linadai linawalenga wanamgambo wa Hamasna limekuwa likijaribu kuepuka kuwadhuru raia. Kulingana na takwimu za mamlaka za Palestina zilizotolewa Jumamosi, mashambulizi ya Israel kwenye ukanda huo yameshawauwa zaidi ya watu 52,000 tangu Okotba 7 mwaka 2023. Idadi ya waliojeruhiwa kwenye vita hivyo ni zaidi ya watu 119,400.