MigogoroAsia
Baada ya gwaride la China, Taiwan yasisitiza amani
3 Septemba 2025Matangazo
Ching te ameyasema hayo muda mfupi baada ya China kufanya gwaride kubwa la maadhimisho ya miaka 80 tangu Japan iliposalimu amri mwishoni mwa vita vya pili vya dunia. Kwa upande wake Lai amelitembelea eneo takatifu la la kitaifa la mashujaa wa Mapinduzi mjini Taipei kama ishara ya heshima kwa wanajeshi waliojitoa muhanga kwa ajili ya taifa hilo. Wachambuzi wanasema gwaride la China katika maadhimisho ya leo lililenga kuonesha uwezo wa kijeshi wa China ikiwa sambamba na washirika wake; Urusi na Korea Kaskazini. Kisiwa cha Taiwan ni eneo linalojitawala wakati China inadai kuwa kisiwa hicho ni eneo lililo chini ya himaya yake na iwapo italazimika itakitwaa kwa nguvu.