TeknolojiaAsia
Taiwan yapiga marufuku DeepSeek ili kulinda usalama wa taifa
1 Februari 2025Matangazo
Wizara inayohusika na masuala ya kidijitali ya Taiwan imesema programu hiyo inahusisha usafirishaji wa taarifa kimataifa na kuzivujisha, na kuwa ina masuala mengine yanayoibua wasiwasi wa kiusalama.
Soma zaidi:Kampuni ya DeepSeek ya China yatikisa soko la hisa la AI
DeepSeek ilianzisha programu ya R1 Chatbot mwezi uliopita na kusema kuwa ina uwezo unaofanana na teknolojia yingine kongwe za akili mnemba za Marekani kwa gharama nafuu zaidi. Kando ya Taiwan, nchi nyingine kama vile Korea Kusini, Ireland, Ufaransa Australia na Italia zimeibua maswali kuhusu mienendo ya kampuni hiyo ya Akili mnemba kutoka China.