TAIPEH: Maandamano kuipinga sheria ya Uchina
26 Machi 2005Matangazo
Elfu kadhaa ya wafanya maandamano wamekusanyika Taipeh,mji mkuu wa Taiwan kuipinga sheria iliyopitishwa na Uchina.Sheria hiyo inaipa Beijing idhini ya kuchukua "hatua zisizo za amani" dhidi ya Taiwan pindi kisiwa hicho kitajiamulia kuwa taifa huru.Rais Chen Shui-bian wa Taiwan anatumai kuwa maandamano hayo yataweza kuihimiza jumuiya ya kimataifa kuishawishi Uchina ifutilie mbali sheria hiyo inayoiruhusu Beijing kutumia nguvu pindi Taiwan itajitenga na Bara.