Asili na mazingiraMarekani
Tahadhari ya joto kali yatolewa mashariki mwa Marekani
24 Juni 2025Matangazo
Wimbi la kwanza la joto kali lilishuhudiwa mwishoni mwa jumaa lililopita huko Marekani huku mamlaka zikitoa tahadhari za kiafya. Hali hiyo inatabiriwa kushuhudiwa hadi siku ya Jumatano katika miji ya Washington, Baltimore, Philadelphia, New York City na Boston.
Hali ya hewa inatarajiwa kufikia nyuzi joto 39 katika kipimo cha Celcius huko New York. Meya wa New York Eric Adams amesema hali hiyo ya joto kali inatarajiwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakaazi, huku akiongeza kuwa kila mwaka joto hugharimu maisha ya watu 500 katika jiji hilo lenye watu milioni nane.