Taarifa za magazeti nchini Uingereza zilihanikiza wiki hii kwamba Ottmar ...
31 Desemba 2003Kwa muujibu wa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ,Hitzfeld ndie kocha bora kabisa wakati huu barani Ulaya na rekodi yake ,alisema inavutia. Hitzfeld ameshinda mara mbili taji la ubingwa nchini Uswisi pamoja na klabu ya Grasshopper ya zurich kabla ya kushika wadhifa wa ukocha wa klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund.Aliongoza Dortmund kutwaa ubingwa wa ujerumani miaka 2 mfululizo 1995 na 1996 na baadae akaitawaza Dortmund klabu bingwa ya ulaya-champions League 1997.
Hitzfeld akashika uskani wa bayern munich-klabu bingwa ya Ujerumani na akaitawaza mabingwa mara 4 mnamo miaka 5 iliopita pamoja na kutwaa ubingwa wa Ulaya-champions League 2001 na Kombe la klabu bingwa duniani mwaka huo. Kuna shida moja katika kumpata Hitzfeld kuachana na klabu yake ya sasa -Bayern Munich.Anasifika kuwa ni mtu anaetimiza ahadi zake anazotoa :Hitzfeld amesema atatimiza mkataba wake na Bayern Munich unaokwenda hadi mwaka 2005.Mazungumzo ya kuurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi yanatarajiwa kufanywa mwaka huu mpya. Mawazo na hisia ziliopo hapa Ujerumani ni kuwa, Ottmar hitzfeld huenda akataka kurithi kiti cha kocha wa sasa wa Ujerumani Rudi Völler baada ya finali za Kombe la dunia 2006 hapa Ujerumani.
THIERRY HENRY AFUTA MACHOZI KWA KUCHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA DIMBA WA MWAKA UFARANSA 2003:
Kati ya wiki hii stadi huyo wa Arsenal london amepiogiwa kura ni mchezaji bora wa dfimba wa Ufaransa na jarida la dimba la Ufaransa.Henry alijipatia kura 162 na kuwashinda mastadi wenzake akina Zinedine Zedane na Ludovic Giuly aliejipatia kura 67 kwa 129 za Zidane. Henry mwenye umri wa miaka 26 alim aliza nafasi ya pili mwaka 2003 kama mchezaji bora wa dimba wa dunia nyuma ya Zidane na akaja wapili tena nyuma ya Pavel Nedved wa jamhuri ya Czech kama mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya.Msimu wa 2003 ,Henry akiichezea Arsenal london na Ufaransa alitia jumla ya mabao 42 katika mechi 64.Katika Ligi ya Uingereza akivaa jazi ya Arsenal London,Henry ametia mabao 25. Katika mapambano 14 ya timu ya taifa ya Ufaransa, henry ametia jumla ya mabao 11 na ndie aliechangia Ufaransa kuilaza simba wa nyika Kamerun kutwaa 2003 Kombe la mashirikisho Confederations Cup. Thierry Henry atakodolewa macho mno Juni hii katika Kombe la Ulaya la mataifa huko Ureno ambako Ufaransa kama mabingwa wa Ulaya watatetea taji lao.
Barani Afrika wiki hii,Tanzania ilipigwa faini au adhabu ya dala 5000 kwa kujitoa katika Kombe la Afrika mashariki na kati Challenge Cup dakika za mwisho huko Sudan-kombe lililotwaliwa n a Uganda.Isitoshe ,Tanzania imepigwa faini ya dala 11.000 kuilipa Sudan, kwa kushindwa Julai mwaka jana kucheza mechi yake huko Omduraman kuania kufuzu kwa kombe la mwezi huu la Afrika la Mataifa nchini Tunisia.
Katika kinyan'ganyiro kinachokuja cha kuania kiti cha rais wa CAF-shirikisho la dimba la Afrika, rais wa sasa wa CAF Issa Hayatou wa Kamerun alitembelea wiki hii Gambia na Ivory Coast kuzishawishi zimuungemkono katika kinyan'ganyiro cha kiti hicho kati yake na Ismail Bhamjee wa Botswana hapo januari 22. Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imemaliza mazowezi yake ya kujiandaa kwa changamoto za mwezi huu za kombe la Afrika la Mataifa nchini Afrika Kusini chini ya kocha wake Muingereza Mick Wadsworth na sasa simba wa Kongo wako nchini Misri wakijiwinda kwa Kombe hilo la Afrika linalochezwa kila baada ya miaka 2 mara hii nchini Tunisia.
KOMBE LA KLABU BINGWA LA AMERIKA KUSINI:
Duru ya kwanza ya Kombe la Libertadores-kombe la klabu bingwa Amerika kusini itaanza Februari 3 kwa mapambano 3.Libertad ya Paraguay itafungua dimba na Deportes ya Colombia mjini Asuncion; Colo Colo ya Chile itaikaribisha Deportivo Cali ya Colombia mjini Santiago. Mabingwa watetezi wa kombe hilo Boca Junuiors ya Argentina itaanza kutetea taji lake kwa changamoto na Bolivar ya Bolivia mjini La Paz hapo Februrari 18. Kombe la klabu bingwa la Amerika kusini limnaaniwa katika makundi 9 ya timu nne-nne mwaka huu.
Klabu ya Ismailia ya Misri, imeomba radhi kwa visa vilivyozuka wakati wa finali ya Kombe la klabu bingwa barania Afrika kati yake na Enyimba ya Nigeria mjini Cairo.Kiasi cha watu 30 walijeruhiwa pale viti vya uwanjani vilipovunjwa,mawe na chupa ziliporushwa na madirisha ya magari na mabasi kuvunjwa.Isitoshe taa za majiani zilivunjwa na miti kuchomwa moto-yote tu kwa kuwa klabu ya nyumnbani haikushinda na Enyimba mabingwa wa Nigeria walitoroka na Kombe hilo kufuatia ushindi wao wa mabao 2:1.
Polisi ya Misri iliwatia nguvuni mashabiki 150.Sherehe ya kuwakabidhi kombe Enyimba iliahirishwa kwa muda wa nusu saa ili uwanja wa mashabiki 20.000 uweze kuhamishwa watazamaji.Ismailia ilijipatia bao la kutatanisha la mkwaju wa penalty lakini kwavile Enyimba ilishinda nyumbani kwa mabao 2:0 katika duru ya kwanza Kombe lilikuwa lao na masdhabiki wa Ismailia hawakuvumilia uchungu huo.Kuomba radhi kwa Ismailia kwa CAF mjini Cairo kulielezea masikitiko kwa ghasia hizo na kwa uongozi mbaya wa mechi ile ilioneshwa moja kwa moja na vituo vya TV barani afrika na Mashariki ya kati. Kisa hiki kinatazamiwa juu ya hivyo kujadiliwa mjini Tunis mwezi huu kabla firimbi kulia kuanzisha kombe la Afrika la Mataifa hapo januari 24.lalamiko la maafisa wa dimba wa Misri kuwa uongozi mbovu wa rifu kutoka Seyschelles Eddy Maillet ndio chanzo cha balaa hilo uwanjani.
RIADHA NA MADHAMBI YA DOPING:
Mwanariadha wa mbio za kasi za mita 100 na 200 wa marekani Kelli White alieshinda masafa hayo katika ubingwa wa riadha wa dunia hapo august nchini Ufaransa ameongoza orodha ya wanariadha 5 wa kimarekani waliogunduliwa na madhambi ya doping wakati wa mashindano ya riadha ya ubingwa wa taifa hapo juni mwaka jana-kamati ya olimpik ya Taifa ya marekani ilifichua kati ya wiki hii.Wengine ni Chryste Gaines,Sandra Glover,Eric Thomas na mrushaji nyundo John McEwen.Jumla wanariadha 7 wa kimarekani na wote wanapanga kukata rufaa. MWAKA WA MICHEZO YA OLIMPIK ATHENS HAPO AUGUST:
Michezo ya Olimpik ya majira ya kiangazi August mwaka huu inarudi kule ilikozaliwa-Ugiriki:Wanaoandaa michezo ya mwaka huu wanakabiliwa na kazi ngumu lakini Kamati ya olimpik ulimwenguni-IOC inahisi kila kitu kinaenda barabara. Ugiriki iliokua nyuma katika maandalio ya michezo hii,imeimarisha juhudi zake za m aandalio na rais wa IOC jacques Rogge amewapongeza waandazi kwa kuhimiza miradi muhimu ya zana za michezo hii kulingana na wakati.Hatahivyo, IOC imewaonya waandazi wa michezo ya Athens kuharakisha matayarisho ili michezo ya olimpik ya mwaka huu istahiki mahala ilikozaliwa. Taarifa za magazeti nchini Uingereza zilihanikiza wiki hii kwamba Ottmar Hitzfeld ndie anaeonekana mtu barabara na chama cha mpira cha Uingereza FA kushika wadhifa huo baada ya kuondoka kwa Eriksson.Mswede eriksson anasemekana huenda akawa kocha wa Chelsea-klabu ilionunuliwa na tajiri mmmoja wa Urusi na ambayo inasimama sasa nafasi ya tatu katika ngazi ya Ligi ya Uingereza nyuma ya Arsenal na Manchester United. Lakini kocha huyo wa Bayern Munich ambae pia wakati mmoja alitajhwa angeliweza kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, amesema na ninamnukulu, "hakuna aliewasiliana nami juu ya swali hilo na sitatakua na hamu sana ya kuchukua kazi hiyo."-alisema Hitzfeld mwenye umri wa miaka 54.
Kwa muujibu wa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ,Hitzfeld ndie kocha bora kabisa wakati huu barani Ulaya na rekodi yake ,alisema inavutia. Hitzfeld ameshinda mara mbili taji la ubingwa nchini Uswisi pamoja na klabu ya Grasshopper ya zurich kabla ya kushika wadhifa wa ukocha wa klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund.Aliongoza Dortmund kutwaa ubingwa wa ujerumani miaka 2 mfululizo 1995 na 1996 na baadae akaitawaza Dortmund klabu bingwa ya ulaya-champions League 1997.
Hitzfeld akashika uskani wa bayern munich-klabu bingwa ya Ujerumani na akaitawaza mabingwa mara 4 mnamo miaka 5 iliopita pamoja na kutwaa ubingwa wa Ulaya-champions League 2001 na Kombe la klabu bingwa duniani mwaka huo. Kuna shida moja katika kumpata Hitzfeld kuachana na klabu yake ya sasa -Bayern Munich.Anasifika kuwa ni mtu anaetimiza ahadi zake anazotoa :Hitzfeld amesema atatimiza mkataba wake na Bayern Munich unaokwenda hadi mwaka 2005.Mazungumzo ya kuurefusha mkataba huo kwa mwaka mmoja zaidi yanatarajiwa kufanywa mwaka huu mpya. Mawazo na hisia ziliopo hapa Ujerumani ni kuwa, Ottmar hitzfeld huenda akataka kurithi kiti cha kocha wa sasa wa Ujerumani Rudi Völler baada ya finali za Kombe la dunia 2006 hapa Ujerumani.
THIERRY HENRY AFUTA MACHOZI KWA KUCHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA DIMBA WA MWAKA UFARANSA 2003:
Kati ya wiki hii stadi huyo wa Arsenal london amepiogiwa kura ni mchezaji bora wa dfimba wa Ufaransa na jarida la dimba la Ufaransa.Henry alijipatia kura 162 na kuwashinda mastadi wenzake akina Zinedine Zedane na Ludovic Giuly aliejipatia kura 67 kwa 129 za Zidane. Henry mwenye umri wa miaka 26 alim aliza nafasi ya pili mwaka 2003 kama mchezaji bora wa dimba wa dunia nyuma ya Zidane na akaja wapili tena nyuma ya Pavel Nedved wa jamhuri ya Czech kama mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya.Msimu wa 2003 ,Henry akiichezea Arsenal london na Ufaransa alitia jumla ya mabao 42 katika mechi 64.Katika Ligi ya Uingereza akivaa jazi ya Arsenal London,Henry ametia mabao 25. Katika mapambano 14 ya timu ya taifa ya Ufaransa, henry ametia jumla ya mabao 11 na ndie aliechangia Ufaransa kuilaza simba wa nyika Kamerun kutwaa 2003 Kombe la mashirikisho Confederations Cup. Thierry Henry atakodolewa macho mno Juni hii katika Kombe la Ulaya la mataifa huko Ureno ambako Ufaransa kama mabingwa wa Ulaya watatetea taji lao.
Barani Afrika wiki hii,Tanzania ilipigwa faini au adhabu ya dala 5000 kwa kujitoa katika Kombe la Afrika mashariki na kati Challenge Cup dakika za mwisho huko Sudan-kombe lililotwaliwa n a Uganda.Isitoshe ,Tanzania imepigwa faini ya dala 11.000 kuilipa Sudan, kwa kushindwa Julai mwaka jana kucheza mechi yake huko Omduraman kuania kufuzu kwa kombe la mwezi huu la Afrika la Mataifa nchini Tunisia.
Katika kinyan'ganyiro kinachokuja cha kuania kiti cha rais wa CAF-shirikisho la dimba la Afrika, rais wa sasa wa CAF Issa Hayatou wa Kamerun alitembelea wiki hii Gambia na Ivory Coast kuzishawishi zimuungemkono katika kinyan'ganyiro cha kiti hicho kati yake na Ismail Bhamjee wa Botswana hapo januari 22. Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imemaliza mazowezi yake ya kujiandaa kwa changamoto za mwezi huu za kombe la Afrika la Mataifa nchini Afrika Kusini chini ya kocha wake Muingereza Mick Wadsworth na sasa simba wa Kongo wako nchini Misri wakijiwinda kwa Kombe hilo la Afrika linalochezwa kila baada ya miaka 2 mara hii nchini Tunisia.
KOMBE LA KLABU BINGWA LA AMERIKA KUSINI:
Duru ya kwanza ya Kombe la Libertadores-kombe la klabu bingwa Amerika kusini itaanza Februari 3 kwa mapambano 3.Libertad ya Paraguay itafungua dimba na Deportes ya Colombia mjini Asuncion; Colo Colo ya Chile itaikaribisha Deportivo Cali ya Colombia mjini Santiago. Mabingwa watetezi wa kombe hilo Boca Junuiors ya Argentina itaanza kutetea taji lake kwa changamoto na Bolivar ya Bolivia mjini La Paz hapo Februrari 18. Kombe la klabu bingwa la Amerika kusini limnaaniwa katika makundi 9 ya timu nne-nne mwaka huu.
Klabu ya Ismailia ya Misri, imeomba radhi kwa visa vilivyozuka wakati wa finali ya Kombe la klabu bingwa barania Afrika kati yake na Enyimba ya Nigeria mjini Cairo.Kiasi cha watu 30 walijeruhiwa pale viti vya uwanjani vilipovunjwa,mawe na chupa ziliporushwa na madirisha ya magari na mabasi kuvunjwa.Isitoshe taa za majiani zilivunjwa na miti kuchomwa moto-yote tu kwa kuwa klabu ya nyumnbani haikushinda na Enyimba mabingwa wa Nigeria walitoroka na Kombe hilo kufuatia ushindi wao wa mabao 2:1.
Polisi ya Misri iliwatia nguvuni mashabiki 150.Sherehe ya kuwakabidhi kombe Enyimba iliahirishwa kwa muda wa nusu saa ili uwanja wa mashabiki 20.000 uweze kuhamishwa watazamaji.Ismailia ilijipatia bao la kutatanisha la mkwaju wa penalty lakini kwavile Enyimba ilishinda nyumbani kwa mabao 2:0 katika duru ya kwanza Kombe lilikuwa lao na masdhabiki wa Ismailia hawakuvumilia uchungu huo.Kuomba radhi kwa Ismailia kwa CAF mjini Cairo kulielezea masikitiko kwa ghasia hizo na kwa uongozi mbaya wa mechi ile ilioneshwa moja kwa moja na vituo vya TV barani afrika na Mashariki ya kati. Kisa hiki kinatazamiwa juu ya hivyo kujadiliwa mjini Tunis mwezi huu kabla firimbi kulia kuanzisha kombe la Afrika la Mataifa hapo januari 24.lalamiko la maafisa wa dimba wa Misri kuwa uongozi mbovu wa rifu kutoka Seyschelles Eddy Maillet ndio chanzo cha balaa hilo uwanjani.
RIADHA NA MADHAMBI YA DOPING:
Mwanariadha wa mbio za kasi za mita 100 na 200 wa marekani Kelli White alieshinda masafa hayo katika ubingwa wa riadha wa dunia hapo august nchini Ufaransa ameongoza orodha ya wanariadha 5 wa kimarekani waliogunduliwa na madhambi ya doping wakati wa mashindano ya riadha ya ubingwa wa taifa hapo juni mwaka jana-kamati ya olimpik ya Taifa ya marekani ilifichua kati ya wiki hii.Wengine ni Chryste Gaines,Sandra Glover,Eric Thomas na mrushaji nyundo John McEwen.Jumla wanariadha 7 wa kimarekani na wote wanapanga kukata rufaa.
MWAKA WA MICHEZO YA OLIMPIK ATHENS HAPO AUGUST:
Michezo ya Olimpik ya majira ya kiangazi August mwaka huu inarudi kule ilikozaliwa-Ugiriki:Wanaoandaa michezo ya mwaka huu wanakabiliwa na kazi ngumu lakini Kamati ya olimpik ulimwenguni-IOC inahisi kila kitu kinaenda barabara. Ugiriki iliokua nyuma katika maandalio ya michezo hii,imeimarisha juhudi zake za m aandalio na rais wa IOC jacques Rogge amewapongeza waandazi kwa kuhimiza miradi muhimu ya zana za michezo hii kulingana na wakati.Hatahivyo, IOC imewaonya waandazi wa michezo ya Athens kuharakisha matayarisho ili michezo ya olimpik ya mwaka huu istahiki mahala ilikozaliwa.