Faraja kama lilivyo jina lake, anayo ari na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko katika jamii kupitia elimu ya afya. Akiwa mwanafunzi wa udaktari, ametumia maarifa anayoyapata chuoni kuelimisha jamii kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanachangia idadi kubwa ya vifo vya watu duniani.