MigogoroSyria
Syria yatangaza usitishwaji mapigano katika jimbo la Sweida
19 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa yake, rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amezitaka pande zote kujitolea kusitisha mara moja mapigano na kumaliza uhasama katika maeneo yote, huku akitahadharisha kuwa ukiukwaji wowote wa hatua hiyo utachukuliwa kama kuingilia uhuru wa taifa hilo.
Msemaji wa wizara ya Mambo ya Ndani Noureddine al-Baba amesema vikosi vya Syria vimeanza kutumwa katika jimbo la Sweida kwa lengo la kuwalinda raia na kukomesha kabisa machafuko.
Siku ya Ijumaa, Kiongozi wa kiroho wa jamii ya Druze, Sheikh Hikmat al-Hijri, alilaani hatua yoyote ya kujaribu kuingia tena kwa vikosi vya serikali katika mkoa huo wa Sweida wanakoishi jamii ya wachache ya Druze waliokabiliana kwa siku kadhaa na ile ya Kibedui .