Syria yaiomba Uturuki msaada wa kuimarisha ulinzi wake
23 Julai 2025Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa wizara ya ulinzi wa Uturuki waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina wakiongeza kuwa Syria imeomba pia msaada wa kukabiliana na "makundi ya kigaidi" ikiwa ni pamoja na lile linalojiita Dola la Kiislamu, IS.
Kwa muda mrefu Uturuki imekuwa ikidhihirisha nia yake ya kuisaidia Syria na imekuwa ikiwapatia maafisa wa nchi hiyo mafunzo, ushauri na msaada wa kiufundi. Mzozo uliibuka kusini mwa Syria wiki iliyopita na kulishuhudiwa mapigano makali kati ya jamii za Bedui na Druze katika jimbo la Sweida.