Syria na Israel wafanya mazungumzo ya ngazi ya juu
20 Agosti 2025Matangazo
Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria, SANA, mazungumzo hayo yamesimamiwa na Marekani ambayo inajaribu kuishawishi Syria isawazishe mahusiano yake ya kidiplomasia na Israel.
Kwenye mkutano huo wa mjini Paris, waziri Al-Shibani alijadiliana na maafisa wa Israel njia za kupunguza misuguano na kurejesha utekelezaji wa mkataba wa kusitisha vita kati ya pande hizo mbili wa mwaka 1974.
Israel na Syria zimetumbukia kwenye uhasama mkubwa hasa tangu Syria ilipopata serikali mpya kufuatia kuangushwa kwa utawala wa Rais Bashar Al-Assad mnamo Disemba mwaka jana.