Mchakato wa uchaguzi wa bunge waahirishwa Syria
23 Agosti 2025Matangazo
Tangazo hili limetolewa na tume ya uchaguzi nchini humo. Uchaguzi huo wa bunge ulikuwa umepangiwa kufanyika tarehe 15 hadi 20 ya mwezi Ujao.
Hakuna tarehe mpa iliyotolewa ya uchaguzi huo kufanyika katika maeneo hayo lakini msemaji wa tume hiyo Hassan al-Daghim amesema uchaguzi utafanyika hali itakaporuhusu.
Waandamanaji mkoani Sweida wataka haki ya kujitawala
Mapema wiki hii rais wa Syria Ahmed al-Sharaa alitia saini mkataba, uliowezesha kupitishwa mabadiliko ya muda katika mfumo wa uchaguzi ambapo sheria hiyo mpya inampa uwezo wa kuteua theluthi moja kati ya wajumbe 210 wa bunge la Syria na theluthi 2 zilizobaki zitachaguliwa na mamlaka za kusimamia uchaguzi nchini humo.