SURA YA UJERUMANI:UHUSIANO WA KIBASLOZI KATI YA UJERUMANI NA ISRASEL UMETIMU MIAKA 40:
21 Januari 2005SURA YA UJERUMANI:
Wakati rais wa Ujerumani Horst Köhler anapanga kuzuru Israel mwanzoni mwa mwezi ujao kuadhimisha mwaka wa 40 tangu Ujerumani na Israel kuanzisha uhusiano wa kibalozi,kuhamia Ujerumani kwa wayahudi kutoka Russia, ni mada inayojadiliwa motomoto wakati huu sawa na vile baadhi ya wabunge wa Israel wanavyobisha kumsikia rais wa Ujerumani wakati wa ziara yake hiyo akihutubia kwa kijerumani katika KNESET-Bunge la Israel.
Uhusiano baina ya nchi hizi mbili kwa jicho la matokeo hayo 2,ndio mada yetu ya leo .Ni Ramadhan Ali tena nikiwakaribisha katika ‘Sura ya Ujerumamni’.
Rais mpya wa Ujerumani Horst Köhler,mwanzoni mwa mwezi ujao atazuru Israel kuadfhimisha na wenyeji wake miaka 40 tangu nchi hizi mbili kuanzisha uhusiano wa kibalozi.Baadhi ya wabunge wa Israel wamedai kwamba rais wa Ujerumani asiruhusdiwe kuhutubia katika KNESET-Bunge la Israel kwa lugha yake ya kijerumani.Akifanya hivyo, wao watasusia na hawatahudhuria kikao hicho.Kwsani, kwa wabunge hao lugha ya kijerumani haitenganiki kabisa na Ujerumani ya Hitler na kuhilikishwa kwa mayahudi wakati wa utawala wa MANAZI.
Rais wa ujerumani kabla ya huyu wa sasa,Johannes Rau utakumbuka alizuru Israel hapo Februari 2000 na alitoa hotuba katika Knesset akiwa rais wa kwanza wa Ujerumani kufanya hivyo,tena kwa lugha yake ya kijerumani.Hata hotuba hii ilisusiwa na baadhi ya wabunge wa Israel.
Spika wa Bunge la Israel REUVEN RIVILIN amelipinga kabisa dai hilo la wabunge hao na akasema haiingii kabisa akilini kwa rais wa Ujerumani kama mgeni wa Israel,asiruhusiwe kuhutubia Bunge kwa luigha yake.
Waziri wa afya wa Israel Dani Naveh, ndie aliezusha mkasa huu wote.Yeye ni mfuasi wa bawa la mrengo wa kulia la chama-tawala cha LIKUD na binafsi ni mtoto wa kiume wa mmoja kati ya wale walionusurika na maisha ya msiba wa kuhilikishwa kwa mayahudi Ujerumani.
Naveh anasema,
"Mama yangu aliekua msichana mdogo alipokabili ghadhabu ya kambi ya manazi ya BERGEN-BELSEN,leo ana umri wa miaka 76.Sauti ya rais wa Ujerumani kutoka jukwaa la Bunge la Israel kwake yeye si sauti ya Heine na Mendelssohn,bali ni sauti ya maafisa wale wa kijeshji ambao walimtisha na kumstusha msichana yule mdogo ambae alitenganishwa na ukoo wake katika kambi ya kuhilikishwa ."
Lakini hata waziri huyu anaelewa vyema kwamba usuhuba mwema ulioimarika kati ya Israel na Ujerumani ambao unaadhimisha mwezi ujao miaka 40 ya mafungamano ya kibalozi,ni wernye umuhimu mkubwa kwa dola ya Israel.Na sio tu mahusiano ya kiuchumi na ushirikiano wa kijeshi ni makubwa mno na ya kuaminiana.Isitoshe,Ujerumani inasimama upande mmoja na Israel katika vikao vyote vya kimataifa.Hatahivyo, adai Naveh,uhusiano kati ya Ujerumani na Israel hauwezi kamwe kuwa wa kawaida.
Anasema zaidi:
"Rais wa Ujerumani bila ya shaka ni mgeni wa kukaribishwa mikono 2 nchini Israel na mahusiano baina ya nchi hizi mbili ni muhimu sana.Lakini,haiwezekani kuyatenganisha kabisa na kile kilichofungamana hapo kabla na uhusiano huu-kile kilichopita."
Bila shaka mtu aweza kuniuliza:Huna heshima mbele ya rais wa ujerumani,rais wa dola rafiki ambae anazuru Israel ?
naamini lakini,tunapaswa kuwa na hisia kabisa za wale waliovuka na maisha kutoka msiba wa holocaust ambao kwao mahusiano baina ya Israel na Ujerumani kamwe haywezi kuwa ya kawaida kama uhusiano na nchi nyengine."
Spika wa Bunge la Israel, REUVLIN RIVLIN alikomesha haraka mjadala huu.Alisema hatatakiwa kabisa rais Köhler,ahutubie kwa lugha nyengine mbali na lugha yake asilia .
Kwahivyo, rais wa Ujerumani, Horst Köhler, atafunga safari mapema m,wezi ujao wa Februari kwa ziara rasmi nchini Israel.Rais Moshe Katsav wa Israel anatazamiwa nae mwezi Mei kuzuru Berlin.Maadhimisho ya miaka 40 tangu nchi hizi mbili kuanzisha usuhuba wa kibalozi yatatukuzwa mwaka huu kwa hafla mbali mbali .Kwa mfano siku ya kuadhimisha Umoja wa Ujerumani-siku nchi 2 za Ujerumani zilipoungana tena-mashariki na magharibi, manuwari ya Ujerumani ‘GORCH FOCK’ itatia gati katika bandari Haifa nchini Israel.
Kuhamia Ujerumani kwa mayahudi kutoka Russia ambao siku za nyuma walifunguliwa m lango wazi,sasa kunaanza kuwa tabu na m,jadala motomoto umeibuka hapa Ujerumani.
Kwa muujibu wa utaratibu uliofuatwa hadi sasa na serikali ya ujerumani kutoka mwaka 1991,wale wote wenye mafungamano na dini ya kiyahudi au alao mzee wao mmoja ni wa asili ya kiyahudi,aliweza kuhamia Ujerumani bila ya pingamizi yoyote.
sasa lakini utaratibu huu unahojiwa na baadhi :
Kiasi cha wayahudi 200.000 kutoka ile iliokua Urusi –Soviet union- walitumia fursa hiyo na kuhamia Ujerumani.Na serikali ya ujerumani inaona hayo ni mafanikio kwavile wahamiaji hao kutoka Ulaya ya mashariki wameweza kuhuyisha jumuia nyingi za wayahudi nchini Ujerumani.Matatizo lakini yamechomoza katika kuwajumuisha wakaazi hao wapya na jamii ya kijerumani.Hii inatokana na ukosefu wa lugha ya kutosha ya kijerumani na ukosefu wa nafasi za kutosha za kazi.
Mawaziri wa ndani wa serikali za mikoa kwahivyo wanyataka sasa kutungwe utaratibu mpya:Wanaomba kuhamia Ujerumani miongoni mwa wakaazi hao wa kiyahudi waweze kukataliwa iwapo kwa kuhamia kwao ujerumani kwa muda mrefu sana watakua wakitegemea ruzuku za misaada ya kuishi kutoka serikalini au malipo ya ukosefu wa kazi.
Wahamiaji ambao watoto wao wamepindukia umri wa miaka 12 na wake au waume zao lazima kwanza wathibitishe wana ujuzi wa kimsingi wa lugha ya kijerumani.Isitoshe hata kabla kuhamia Ujerumani, mayahudi hao wa