SURA YA UJERUMANI:
25 Februari 2005Mkataba juu ya Katiba ya Umoja wa ulaya ingawa ulikwishatiwa saini kati ya mwaka jana,kuidhinishwa kwake kumefanywa hadi sasa na nchi tatu zanachama:Lithuania,Slovenia na Hungary.Majuzi hivi,Spian ilijiunga na safu hiyo kuwa nchi ya 4 kuidhinisha katiba hiyo ya UM.
Serikali ya Ujerumani ina azma halkadhalika kuidhinisha katiba hiyo ya UU,lakini bila ya kuitisha kwanza kura ya maoni kuwauliza wananchi.Inapanga kuiwasilisha Bungeni kuidhinishwa.Alhamisi ya tarehe 24-Februari,m,jadala wa kwanza ulifanyika Bungeni kuhusu katiba ya Umoja wa Ulaya huku muungano wa vyama vya Upinzani wa CDU/CSU ingawa unaungamkono katiba hiyo na utayari kuiidhinisha,hatahivyo, unataka kupewa sauti katika swali hili-jambo ambalo serikali ya muungano wa vyama vya SPD na walinzi wa mazingira –KIJANI hawako tayari kuridhia.
Halkadhalika wiki hii,Bibi Gesine Schwan,aliegombea wadhifa wa urais mwaka jana kwa tiketi ya chama-tawala cha SPD na kushindwa na rais wa sasa Horst Köhler,ametunzwa nishani ya Ujerumani ya ‘mwanamke bora kabisa wa Ulaya 2005".
SURA YA UJERUMANI itawapa sura halisi ya bibi huyu na ilikuaje kupewa nishani hiyo.
Muungano wa vyama vya Upinzani wa CDU/CSU utaiidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya na hakuna shaka juu ya jambo hilo.hii imefafanuliwa wazi namsemaji wa muungano huo anaehusika na siasa za nje Bw.Wolfgang Schauble mwanzoni mwa mashauriano ya wanabunge.Upinzani lakini unadai sauti kubwa kupewa Bunge yxa kuamua kile ambacho kimeptishwa na Umoja wa Ulaya mjini Brussels,Ubelgiji.
Bw.Schauble asema,
"Ni ukweli pia wananchi waweza kujumuishwa na uamuzi ikiwa mabunge ya kitaifa yanashirikishwa mapema na swali hili.
La si hivyo, mambo yataenda kombo.Kuanzia mwongozo uliopitishwa wa kupinga ubaguzi hadi uongozaji huduma tunajionea hivi sasa kinachotokea ikiwa wananchi hawakushirikishwa na mapema katika kuamua mambo yanayopangwa kutendeka Ulaya."
Muungano huo unadai kwahivyo Bunge la Ujerumani –Bundestag kuwa na kauli katika kuidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya kabla uamuzi wa mwisho kupitishwa Brussels.
Serikali ya muungano ya vyama vya SPD na KIJANI inakataa kuitikia ombi hilo alao hadi sasa.Lakini sio tu vyama hivyo tawala, lakini vinaungwamkono na chama kingione cha Upinzani cha Free Democratic Party.
Msemaji wa chama hiki waziri wa zamani wa sheria,bibi Sabine Leuthäuser-Schnarrenberger amesema ,kuridhia kutoa sauti kubwa kwa Bunge kutaifunga kamba serikali yoyote bila kujali ni ya chama gani katika kupitisha uamuzi.
Anasema,
"Haiwezi kuwa serikali ya Ujerumani inafungwa kambna na kubidi kutumia simu tu na kuliuliza Bunge iwapo inaruhusiwa kusema hili au lile au wakati wa majadiliano ni ruhusa kutamka hili au lile au kwanza inabidi kurudi bungeni kuuliza."
Waziri wa nje wa Ujerumani,Bw.Joshka Fischer, anaona upo uwezekano katika maswali ya utata kushauriana na Upinzani na kuridhiana nao.Na hasa katika maswali jinsi gani uamuzi wa pamoja kati ya Bunge la shirikisho na lile la mikoa-Bundestag na Bundesrat.
Ili kuidhinishwa katiba ya Umoja wa Ulaya panahitajika wingi wa thuluthi-mbili tena tangu katika Bunge la shirikisho hata lile la mikoa.
Katiba ya UU ni nguzo ya kusimamia Umoja wa Ulaya na ndio jiwe la msingi la kuzidi kwa ushawishi katika siasa za nje za UU-asema waziri wa nje wa Ujerumani-Joshka Fischer.
Waziri Fischer asema,"Nikiangalia katiba hii ina maana gani kwa raia wa Ulaya,nikiangalia katiba hii ina umuhimu gani pia kwa Umoja wa Ulaya katika jukumu lake linaloongezeka la sera za nje na ulinzi,sina budi kusaisitiza kwamba, tunahitaji katiba hii na kwahivyo, natumai Bunge la Ujerumani kwa wingi mkubwa na haraka kama iwezekanavyo litaidhinisha katiba hii."
Serikali ya Ujerumani kwa kuidhinishwa haraka katiba ya UU ingependa kutoa ishara kwa zile nchi za Ulaya ambazo kuidhinshwa kwa katiba hiyo hakuhitaji kama ujerumani kura ya maoni.
Miongoni mwa nchi kama hizo, ni jirani Ufaransa ambako kuidhinisha katiba hii bado kuna shaka shaka.
Tugeukie sasa mada yetu ya pili:NANI BIBI GESINE SCHWAN NA ILIKUAJE AKATUNZWA NISHANI YA UJERUMANI YA MWANMKE BORA BARANI ULAYA ?
Mtaalamu huyu wa fani ya siasa-Gesine Schwan ,wiki hii alitunzwa nishani ya "Mwanamke wa Ulaya ya 2005’ inayotolewa na Ujerumani.
Yeye na rais wa chuo kikuu cha VIADRINA m huko Frankfurt/Order.Alitunzwa nishani hiyo kwa juhudi zake zisizochoka na mchango wake wa kupalilia urafiki mwema tangu miaka 30 sasa kati ya Ujerumani na Poland.
Gesine Schwan, hafahamiki na kutambulika bali pia muda mrefu sasa anachangia mno kupalilia usuhuba mwema kati ya wajerumani na wapoland.
profesa huyu wa sayansi ya kisiasa anazungumza kipoland kwa ufasaha na baada ya kujifunza mjini warsaw na Krakau alihetimu mafunzo yake chini ya mtaalamu wa falsafa wa kipoland Leszek Kolakowski.
Bibi Gesine schwan ,mzaliwa wa Berlin, mara kwa mara husafiri kwenda Poland na anafanya kazi katika mji wa Frankfurt/Order unaopakana na Poland.huko bibi Schwan ni rais wa Chuo kikuu cha Ulaya cha VIADRINA ambamo thuluthi-moja ya wanafunzi wake ni wapoland.Kwa moani yake wajerumani na wapoland wataweza tu kufahamiana uzuiri zaidi iwapo idadi ya mikutano kati yao ikiongezeka mno.
Anasema bibi Schwan:
"Kwa kadri hamjuani,ndipo mtu huchupa haraka kuwa na dhana zisizoza kweli juu ya mwenzake .pale mtu akijua barabara hisia za mwenzake basi ndipo yawezekana kumuelewa na kujongeleana na mara nyingi huibuka mafahamiano mema."
Katika chuo kikuu cha VIADRINA, Bibi Schwan anasukuma mbele shughuli ndogo-ndogo kuhimiza na kupalilia usuhuba mwema na jirani Poland na karibuni atajitwika jukumu hata kubwa zaisdi upande huo.Kwani, serikali ya ujerumani inaambatisha umuhimu mkubwa kuona Chuo Kikuu cha VIADRINA kinageuka Wakfu unaogharimiwa kwa kima cha Euro milioni 50.Bibi Gesine Schwan amejitwika dhamana hii mpya ya kuongoza wakfu huo mbali na jukumu lake kama mwenyekiti wa chuo kikuu hicho.
Wadhifa huu uko chini ya wizara ya nje.
Bibi ghesine Schwan anapanga kwanza kuzungumza na waziri wa ndani na mwenzake wa poland.Isitoshe, ana azma ya kuzitupia jicho juhudi mbali mbali zinazopalilia maingiliano mema kati ya wajerumani na wapoland.
Msocial-democrat huyu Gesine Schwan ,utaklumbuka mwaka uliopita aliteuliwa na chama chake cha SPD kugombea wadhifa wa urais wa Ujerumani na alipambana na rais wa sasa Horst Köhler.Alishindwa katika uchaguzi huo kwavile chama chake hakikua na wingi wa kura Bungeni.
Anajulikana kwa kusema wazi wazi anachofikiri na amebainisha wazi kwamba amejitwika jukumu jipya alilopewa baada ya kufikiri sana na kusita sita.Kwani, tayari amebeba mzigo mzito akiwa rais wa Chuo Kikuu cha VIADRINA.
Amepania hatahivyo, kuwa mtetezi mkubwa nchini Ujerumani wa uhusiano bora kati ya wajerumani na jirani zao wapoland.