Wakati athari za vita vya Urusi Ukraine zikianza kuzilemea chumi za Ulaya, Ujerumani ni miongoni mwa walioathirika. Kampuni ya uuzaji gesi ya Urusi, Gazprom, ilipunguza usafirishaji wa gesi katika bomba la Nord Stream 1 kwa asilimia zaidi ya 60 kuelekea Ujerumani. Kampuni ya kutengeneza glasi za manukato Heinz Glas inasema hali ikiendelea hivi haitoweza kutengeneza glasi. Msikilize Amina Abubakar.