Sumatra, Indonesia. Waandamanaji wachoma majengo na magari wakikasirishwa na uchaguzi wa serikali za mitaa.
25 Julai 2005Matangazo
Maelfu ya waandamanaji wenye hasira wamechoma moto majengo na magari katika mji wa Bintuhan ulioko katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia.
Waandamanaji hao walikuwa wanaandamana dhidi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao wanadai ulijaa udanganyifu.
Polisi wamesema kuwa waandamanaji huenda walianza kufanya ghasia baada ya maafisa wa eneo hilo kushindwa kukutana nao ili kujadili madai hayo ya udanganyifu.
Mwezi uliopita , Waindonesia kwa mara ya kwanza walipiga kura kuwachagua maafisa wao wa serikali za mitaa kama mkuu wa wilaya, meya na magavana.