JangaAfrika
Sudan yaomba kusaidiwa kukabiliana na athari za maporomoko
3 Septemba 2025Matangazo
Kiongozi wa kundi la waasi wa Jeshi la Ukombozi la Sudan Abdel-Wahid Nour vinavyolidhibiti eneo hilo, amesema ukubwa wa janga hilo hauelezeki na ameutaka Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada kusaidia kuipata miili ya watu ambayo bado haijapatikana.
Mtu mmoja pekee ndiye aliyesalimika katika kijiji kizima cha Tarasin kilicho kwenye eneo la milima ya Jebel Marra kilichokumbwa na janga hilo. Kwa upande wake mratibu wa misaada ya kiutu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Luca Renda, amesema anashirikiana na washirika wa umoja huo kuratibu usaidizi kwa jamii zilizoathiriwa