MigogoroAfrika
Sudan: Kenya inasambaza silaha kwa kundi la RSF
25 Juni 2025Matangazo
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema katika taarifa yake kuwa mwezi uliopita, jeshi liligundua katika maficho ya silaha za wanamgambo wa RSF mjini Khartoum, silaha na risasi zilizoonekana kuwa na maandishi kwamba zilitokea nchini Kenya.
Tangu kuanza kwa mzozo huo Aprili mwaka 2023, jeshi la Sudan linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF chini ya uongozi wa Mohamed Hamdan Daglo wamekuwa wakishtumiana kupokea silaha kutoka kwa mataifa ya kigeni, kama Umoja wa Falme za kiarabu (UAE), Misri, Iran, Uturuki na Urusi.