Sudan na UAE, kupambana katika mahakama ya ICJ
10 Aprili 2025Matangazo
Katika ombi lake kwenye mahakama hiyo, Sudan imesema kuwa waasi wa RSF, kwa msaada usio na kikomo wa Umoja wa Falme za Kiarabu, walifanya mauaji ya halaiki, kuwahamisha watu kwa nguvu pamoja na mauaji.
Imewataka majaji kuiamuru UAE kuwafidia waathiriwa wa vita nchini Sudan.
UAE yasema madai ya Sudan hayana msingi
Lakini kwa upande wake, afisa mmoja mkuu wa Umoja huo wa Falme za Kiarabu aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba madai hayo hayana msingi na ni matumizi mabaya ya muda na shughuli za mahakama hiyo.
UAE imekanusha kusambaza silaha kwa RSF.