Sudan Kusini yamkubalia raia wa Kongo aliyefukuzwa Marekani
9 Aprili 2025Wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini ilisema mzozo huo ulitokana na kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyefukuzwa Marekani na kupelekwa Juba mapema Aprili alitumia jina la uongo.
Ni kwa sababu hiyo ambapo alirudishwa Marekani. Lakini wizara hiyo sasa imesema kuwa kwa mujibu wa uhusiano wa kirafiki kati ya Sudan Kusini na Marekani, serikali imeamua kumruhusu" raia huyu wa Kongo kuingia katika ardhi yake. Imesema imewataka maafisa katika uwanja wa ndege wa Juba kushughulikia kuwasili kwake Jumatano.
Mjini Washington, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Tammy Bruce amesema Marekani itaisubiri Sudan Kusini kutekeleza ilichokisema katika taarifa hiyo. Kisha watatathmini kwa mara nyingine hatua walizochukua wakati Sudan Kusini itakaposhirikiana kikamilifu.