Sudan Kusini yahimiza mazungumzo kuhusu visa za Marekani
8 Aprili 2025Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini imesema nchi hiyo inakabiliwa na kile ilichosema ni "kufutwa kwa viza kwa msingi wa tukio la pekee linalohusisha upotoshaji wa mtu ambaye si raia wa Sudan Kusini". Kisa hicho kilimhusisha mtu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyefukuzwa Marekani na kurejeshwa Sudan Kusini, lakini akazuiwa kuingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba Aprili 5 na 6.
Taarifa hiyo imesema Sudan Kusini "inaendelea kuwa thabiti katika dhamira yake ya kusuluhisha suala hili kupitia mazungumzo yenye kujenga na ushirikiano" kwa namna "inayoendana na viwango na sheria za kimataifa." Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio alisema Jumapili kuwa Juba inaitumia vibaya Marekani, akilalamika kuwa Sudan Kusini haiwapokei raia wake waliofukuzwa Marekani.