Sudan Kusini: Mshirika mwingine wa Machar akamatwa
7 Machi 2025Wiki hii, waziri wa mafuta na naibu mkuu wa jeshi ambao pia ni washirika wa Machar.
Kukamatwa kwa watu hao kumeibua wasiwasi kuhusu kuvunjika kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2018 kati ya Rais Salva Kiir na Machar ambayo yaliwezesha kumaliza vita miaka mitano vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 400,000.
Soma pia: Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi wa Desemba kwa miaka miwili
Mvutano huo unaoongezeka kati ya viongozi hao umetishia kusambaratika kwa serikali ya umoja wa kitaifa, huku mapigano makali yakiripotiwa katika jimbo la kaskazini mashariki la Upper Nile ambako serikali ya Sudan Kusini inasema jeshi linakabiliana na waasi wanaoungwa mkono na vikosi vya Machar.
Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kuongezeka kwa mapigano hayo yanayohusisha matumizi ya "silaha nzito" na vifo vingi.