Sudan: Jeshi lakomboa sehemu kubwa ya jiji la Khartoum
9 Februari 2025Matangazo
Kwenye taarifa yake Jeshi la Sudan limesema linazidisha mashambulizi yake kwa lengo la kurudisha udhibiti kamili wa mji mkuu huo kutoka kwa vikosi vya wa RSF. Katikati ya mafanikio hayo, kiongozi mkuu wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan, ametangaza mipango ya kuunda serikali ya mpito itakayosaidia kukamilisha kazi zilizosalia za jeshi katika kuikomboa Sudan kutoka kwenye mikono ya vikosi vilivyoasi vya RSF.