STRASBOURG: Uturuki isawazishe uhusiano na Cyprus
27 Septemba 2006Matangazo
Uturuki imeonywa na Bunge la Ulaya juu ya uwezekano wa kuvunjwa majadiliano yanayoendelea hivi sasa ya kutaka kujiunga katika Umoja wa nchi za Ulaya pindi hadi mwisho wa mwaka huu,Uturuki haitoondosha vikwazo vyake dhidi ya meli za Cyprus.Bunge la Ulaya limeamua kuwa Uturuki inapaswa kuchukua hatua za kusawazisha uhusiano wake na Cyprus au utaratibu wa majadiliano utaweza kukwama.Wakati huo huo Bunge la Ulaya limeituhumu Uturuki kuwa hamu ya kufanya mageuzi yaonekana kuwa ndogo na haki za binadamu zinaendelea kukiukwa.Hali ya mambo hasa hairidhishi upande wa uhuru wa usemi.