STRALSUND: Bush amaliza ziara nchini Ujerumani
14 Julai 2006Matangazo
Rais George W.Bush wa Marekani hii leo amekamilisha ziara yake nchini Ujerumani na ameelekea St.Petersburg nchini Urussi kuhudhuria mkutano wa madola tajiri G-8.Bush na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani baada ya mazungumzo yap,walikuwa na msimamo mmoja kuhusu migogoro ya kimataifa.Vile vile walisisitiza uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya Marekani na Ujerumani.Viongozi hao wawili vile vile walieleza wasi wasi wao kuhusu hali ya Mashariki ya Kati inayozidi kuwa tete.Na kuhusu suala la Iran,Bush na Merkel wameitaka Teheran upesi itoe jawabu lake kuhusiana na mapendekezo yaliyotolewa na jumuiya ya kimataifa.