Steve Witkoff kuzuru Ulaya na Mashariki ya Kati
23 Julai 2025Matangazo
Marekani imesema mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Mashariki ya Kati Steve Witkoff atazuru Ulaya kwa mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano na kukamilisha mchakato wa kutenga ukanda wa kupitishia misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ambako mamlaka wanasema watu wanakufa kutokana na njaa.
Witkoff, mjumbe wa rais Donald Trump, atakwenda Mashariki ya Kati baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya.
Msemaji wa wziara ya mambo ya nje ya Marekani Tammy Bruce amesema Witkoff atazuru Ulaya na matumaini makubwa ya kupata makubaliano ya usitishaji mapigano pamoja na kutengwa kwa eneo hilo la kupitishia misaada, jambo ambalo pande zote zimekubaliana.
Bruce hata hivyo hakutoa taarifa zaidi kuhusu eneo hilo la kupitishia misaada.