Steinmeier ziarani Mashariki ya Kati
3 Februari 2025Matangazo
Taarifa ya ofisi yake imesema Steinmeier amepangiwa kukutana na Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia leo mjini Riyadh.
Hapo kesho atakwenda nchini Jordan kwa mazungumzo na Mfalme Abdullah II na kisha kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani kwenye kambi ya al-Azraq.
Soma pia:
Vikosi vya Ujerumani viko nchini Jordan chini ya mwavuli wa ujumbe wa kimataifa wa kupambana na kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu.
Mnamo siku ya Jumatano, Rais Steinmeier atahitimisha ziara yake kwa kuitembelea Uturuki kujadili hali ya Syria na mwenzakeb Rais Recep Tayyip Erdogan.