MigogoroUingereza
Starmer amuunga mkono Zelensky, akosoa matamshi ya Trump
20 Februari 2025Matangazo
Waziri Mkuu Starmer amezungumza kwa simu na Zelensky na kumwambia anamuunga mkono kama kiongozi wa Ukraine aliyechaguliwa kidemokrasia na kuongeza kuwa ilikuwa ni busara kutofanya uchaguzi wakati wa vita na kwamba Uingereza ilifanya hivyo wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa ofisi yake ya Downing Street.
Trump amemkosoa kiongozi mwenzake kwa kusitisha uchaguzi na kudai kwamba Ukraine ndio ilivianzisha vita na Urusi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameliambia gazeti la Der Spiegel kwamba matamshi hayo potofu na hatari dhidi ya Rais Zelensky, aliyeko madarakani kulingana na sheria za nchi.